Connect with us

Makala

Songombingo Usajili wa Kibu

Mshambuliaji wa klabu ya Simba sc Kibu Dennis ameendelea kushika vichwa vya habari za usajili nchini kutokana na kuelekea kumaliza mkataba wake na klabu ya Simba sc ambapo baadhi ya klabu kubwa nchini zinatajwa kuwania saini yake.

Kibu mwenye asili ya nchini Congo Drc anatajwa kuhitajika na klabu ya Yanga sc,Simba sc ambapo alipo mpaka sasa sambamba na Ihefu Fc huku Azam Fc nayo ikitajwa kumhitaji japo haipo siriazi sana.

Kibu ambaye alijiunga na Simba sc msimu wa 2022/2023 kwa mkataba wa miaka miwili ambapo mkataba huo unaisha mwezi juni mwaka huu na amekaa na klabu yake hiyo ambapo amehitaji kiasi cha shilingi milioni mia tatu za pamoja kama dau la usajili na mshahara wa shilingi milioni 15 ambazo mpaka sasa klabu hiyo imekubali kumpa kwa sharti la kulipwa kwa mafungu mawili ama zaidi kitu ambacho mchezaji huyo hataki.

Yanga sc wenyewe wako tayari kumpa Kibu mkataba wa miaka miwili wenye dau la shilingi milioni mia tatu kama pesa ya usajili kwa miaka miwili na mshahara wa milioni 15 kama Simba sc lakini Kibu anavutiwa na Yanga sc kutokana na bonansi ambazo hutoa hasa katika michuano ya kimataifa.

Ihefu Fc nao wameonesha nia ya kumsajili mchezaji huyo lakini yenyewe imempa mkataba wa dau la shilingi milioni mia tano kwa miaka mitatu ambazo pia zitalipwa kwa mafungu kitu ambacho Kibu mpaka sasa hajakubaliana nacho akitoa macho zaidi ofa ya Yanga sc ama Simba sc.

Kinacholeta uzito kukamilisha madili hayo ni takwimu za mchezaji husika ambapo katika mechi 20 amefunga bao moja pekee msimu huu ambalo amewafunga Yanga sc walipofungwa 5-1 ambapo msimu uliopita katika ligi kuu alifunga mabao manne na kutoa assisti nne pekee hali ambayo Simba sc wanajiuliza kama anastahili dau hilo.

Baadhi ya klabu hizo pamoja na kuonyesha nia ya kumsajili staa huyo bado zinaangalia na upepo ili zisije kukurupuka kulipa hela kubwa kutokana na biashara hiyo kuvamiwa na wapige debe wa mchezaji huyo ambao wanazusha ofa zingine ili kumuongezea thamani staa huyo.

Hati hivyo ni ngumu kupata mchezaji mzawa mwenye hali ya upambanaji kama ya Kibu Dennis pamoja na kwamba hafungi lakini husaidia timu kimuunda hasa wakati wa kushambulia pamoja na kukaba huku pia akiwa na nidhamu binafsi tofauti na mastaa wengi hasa wakianza kushika fedha.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala