Connect with us

Makala

Yanga Sc Yajichimbia Kileleni

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuibuka na alama tatu muhimu baada ya kuifunga Kagera Sugar Fc bao 1-0 katika mchezo wa raundi ya 26 ya ligi kuu ya Nbc nchini uliofanyika katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam.

Yanga sc ikianza na mshambuliaji mmoja Joseph Guede ilishindwa kuziona nyavu za Kagera Sugar licha ya kushambulia mara kwa mara  kupitia kwa Stephane Aziz Ki na Pacome Zouzou ambapo walinzi wa Kagera Sugar sambamba na viungo waliamua kukaba zaidi hasa eneo la 18 ya upande wao.

Azizi Ki mwenye magoli 15 ya ligi kuu alijitahidi kutafuta bao ili kuongeza idadi ya magoli lakini uimara wa safu ya ulinzi ya Kagera Sugar ulikua kikwazo na kusubiri hadi dakika ya 83 ambapo alitoa usaidizi wa upatikanaji wa bao kwa pasi nzuri na Mudathir Yahya Abass kufunga bao pekee la ushindi.

Joseph Guede alifunga bao la pili kwa Yanga sc dakika ya 88 lakini mshika kibendera aliashiria kwamba ameotea japo picha za marejeo zilionyesha kuwa lilikua ni bao sahihi.

Yanga sc sasa imefikisha alama 68 kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini ikicheza michezo 26 na inahitaji alama nne pekee kuwa mabingwa wa ligi kuu kwa mara ya 30 huku Kagera Sugar wakiwa na alama 30 katika nafasi ya saba ya msimamo wa ligi kuu nchini baada ya kucheza michezo 26.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala