Connect with us

Makala

Manchester City 2021/2022

Klabu ya Manchester City imefanikiwa kutwaa taji la sita la ligi kuu ya Uingereza baada ya kuifunga timu ya Aston Villa 3-2 katika uwanja wa nyumbani wa Ettihad na kuwaacha Liverpool wakishangaa baada ya kulikosa taji hilo.

Mpaka dakika ya 74 Manchester City walikua nyuma kwa mabao mawili ya Matty Cash 37′ na Philipe Coutinho 69′ ambapo ilimlazimu Pep Guardiola kumuingiza kiungo Ikay Gundogan aliyefungua ukurasa wa mabao dakika ya 76 kisha kiungo Rodri akafunga la kusawazisha dakika ya 78 huku Gundogan tena akifunga bao la ushindi dakika ya 81 na kuihakikishia Man City ubingwa wa Epl kwa kufikisha alama 93 huku Liverpool wakiwa na alama 92.

Pep Guardiola sasa amefanikiwa kuipa Man city makombe manne ya ligi kuu katika misimu mitano aliyokaa klabuni hapo huku akifanikiwa kuchukua taji hilo mara tatu mfululizo.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala