Connect with us

Makala

Chanzo Manula Kuikosa Geita Fc

Dakika chache kabla ya kuanza kwa mchezo wa klabu ya Simba sc dhidi ya Geita Gold FC, mlinda mlango  Aishi Manula aliumia mkono baada ya kukatwa na kioo katika chumba cha kubadilishia nguo (dressing room) cha wachezaji wa klabu hiyo katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza.
Manula aliwasili uwanja wa CCM Kirumba akiwa kwenye orodha ya wachezaji wanaocheza mchezo huo na baada ya kuingia katika chumba cha kubadilishia nguo akaangukiwa na kioo ambacho kilivunjika baada ya kuegemewa na mashabiki waliokua nje chumba hicho na hivyo kulazimika kuwekwa pembeni huku Kipa Benno Kakolanya na Ally Salim wakaingizwa kikosini.
Licha ya Manula kukosekana katika mchezo huo ulioisha kwa sare ya 1-1 kipa Kakolanya alifanya vizuri na kuiweka Simba sc mchezoni mara kwa mara kutokana na kuokoa mashambulizi kadhaa langoni hapo.
Aishi alipatiwa matibabu na anaendelea vizuri huku ikitazamwa hali yake kuelekea mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya klabu ya Yanga sc kuangalia kama anaweza kutumika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala