Connect with us

Makala

Yanga sc Yabakisha 3 Ubingwa

Baada ya kutoa sare ya 1-1 na klabu ya Biashara United sasa klabu ya Yanga sc imebakisha alama tatu pekee ili kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa ligi kuu ya soka ya Nbc nchini.

Licha ya mshambuliaji Fiston Mayele kutetema dakika ya 74 ya mchezo bao hilo halikudumu kwani Collin Opare alisawazisha bao hilo dakika ya 77 baada ya beki Bakari Mwamnyeto kufanya makosa ya kutokaba krosi iliyomkuta mfungaji akiwa mwenyewe na kumchambua kipa Aboutwalib Mshery.

Kipindi cha kwanza Yanga sc watakijutia baada ya kukosa nafasi nyingi ambazo walizitengeneza kupitia kwa Chico Ushindi na Dickson Ambundo ambao walikua wanakosa utulivu na kusababisha mchezo kuwa mgumu hasa kipindi cha pili.

Kutokana na ushindi huo Yanga sc sasa imefikisha alama 64 ikihitaji alama tatu pekee ili kufikisha alama 67 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yeyote huku pia ikiwa na wastani mkubwa wa mabao ya kufunga na kufungwa tofauti na Simba sc wenye alama 51 huku ikiwa na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa 21.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala