Connect with us

Makala

Yanga sc Yakimbia Jiji Mwanza

Baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Biashara United klabu ya Yanga sc leo mapema imehamishia kambi yake mkoani Shinyanga kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba sc utakaofanyika katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini humo.

Yanga sc ikiwa na kikosi chake kamili ilisafiri mpaka mkoani humo na kupokelewa na mashabiki wa klabu hiyo katika eneo la Maganzo ambao waliwasindikiza mpaka hotelini huku Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Fredrick Mwakalebela akisema kuwa kambi hiyo ni mpango mkakati wa ushindi siku ya Jumamosi.

“Tumesikia taarifa za Simba kuendelea kubakia Mwanza mara baada ya mchezo wao wa ligi wa leo (jana) dhidi ya Geita Gold kujiandaa na nusu fainali ya FA ambayo itachezwa CCM Kirumba.

“Hivyo sisi hatutaendelea kukaa hapa na badala yake timu itaelekea Shinyanga mara tu baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Biashara kumalizika ili tujiandae kwa nafasi zaidi.

“Kama unavyofahamu, dabi inapokaribia maandalizi yanatakiwa yafanywe kwa usiri mkubwa, lazima makocha wetu wachague sehemu nzuri watakayofanya maandalizi,” alisema Mwakalebela.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala