Connect with us

Makala

Saido,Ambudo Watimuliwa Yanga sc

Taarifa kutoka mkoani Shinyanga zinasema kuwa klabu ya Yanga sc imewatimua kambini mastaa wake Saido Ntibanzokiza na Dickson Ambundo kwa kosa la kuondoka kambini bila kufuata utaratibu uliowekwa na klabu wakati timu ikiwa kambini mkoani Mwanza kabla ya mchezo dhidi ya Biashara united.

Taarifa za kutimuliwa kambini ikiwa ni siku mbili kabla kuwavaa mahasimu wao Simba sc katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la shirikisho nchini utakaofanyika katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza.

Uamuzi huo wa kuwatimua mastaa hao umefikiwa na kocha mkuu wa klabu hiyo Nasredine Mohamed Nabi ili kuweka nidhamu sawa kwa mastaa wote wa timu hiyo linapokuja suala la kufuata taratibu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala