Klabu ya Barcelona Fc imeibuka mabingwa wa kombe la mfalme la nchini Hispania (Copa De La Rey) baada ya kuifunga timu ya Real Madrid kwa mabao 3-2 katika mchezo mkali uliochezwa katika uwanja wa Estadio de la Cartuja uliopo mjini Sevila nchini humo.
Real Madrid kinyume na ilivyotarajiwa na wengi ilijikuta ikiruhusu bao la mapema baada ya mabeki kuzembe kumkaba Lamine Yamal aliyetoa pasi kwa Pedri amabye alipiga shuti kali lilimshinda kipa na kuingia wavuni moja kwa moja.
Kyllian Mbape alifunga bao la kusawazisha kwa mpira wa faulo dakika ya 70 huku dakika saba baadae Aurelien Tchouamen akifunga kwa kichwa na kuipa uongozi Real Madrid lakini kinyume na matarajio ya wengi dakika ya 83 makosa ya kipa Wojciech Szczesny na mlindi Antonio Rudiger yaliwapa Barcelona bao la kusawazisha kupitia kwa Ferran Torres.
Baada ya dakika 90 kumalizika kwa matokeo ya 2-2 ililazimika kuongezwa kwa dakika 30 kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo ambapo Barcelona walifanikiwa kupata bao la tatu kwa shuti kali la Jules Kounde dakika ya 116 ya mchezo na kuipa ubingwa Barcelona.
Katika mchezo huo wachezaji watatu wa Real Madrid Jude Bellingham,Lucas Vazquez na Antonio Rudiger walionyeshwa kadi nyekundi kwa mkupuo kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu.