Home Makala Simba Sc Kuvaa Diadora ya Italia

Simba Sc Kuvaa Diadora ya Italia

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba Sc sasa rasmi itavaa nembo ya mavazi ya Diadora kuanzia msimu ujao katika vifaa vyote vya mazoezi na mechi pamoja na hafla rasmi za klabu hiyo baada ya kuingia makubaliano rasmi kupitia kampuni ya Jayrutty Investment Company.

Awali katika kusaini mikataba ya mavazi na kampuni hiyo ya Jayrutty Investment Company Limited ambapo Mkurugenzi wa kampuni hiyo Cpa.Joseph Rwagasira alisema kuwa atailetea klabu hiyo kampuni kubwa kwa ajili ya mavazi rasmi ya klabu.

banner

“Wakati tunatangazwa kuingia mkataba huu na kutengeneza vifaa vya Simba kuanzia msimu ujao niliahidi. Kutokana na ukubwa wa Simba ni wakati wa kwenda kimataifa na leo tupo makao makuu ya Diadora ukanda wa SADEC na kwa mara ya kwanza tunakwenda kutangaza ushiriki wa pamoja kati ya Simba, Jayrutty na Diadora.” Alisema Afisa Mtendaji Mkuu wa Jayrutty, Joseph Rwegasira.

Nao kampuni ya Diadora ambao wana tawi maalumu Afrika ya kusini ambayo inafanya kazi mpaka nchi za jumuiya ya Sadc walisema kuwa wanafuraha kukamilisha dili hilo na klabu inayofanya vizuri barani Afrika.

“Tumefurahi kupata nafasi hii ya kuwa sehemu ya udhamini wa miongoni mwa klabu kubwa Afrika na tunahidi kwenda kutengeneza bidhaa bora kama ilivyokuwa kwa timu tulizowahi kuzivalisha kwa muda mrefu ikiwemo AS Roma ya Italy.”- Afisa Mtendaji Mkuu Diadora, Mr. Yusuf Vadi.

Tayari mabosi wa klabu hiyo wapo nchini Afrika ya kusini ambapo Mwenyekiti wa klabu hiyo Mh.Murtaza Mangungu alisema kuwa hiyo ni fursa kubwa kwa klabu hiyo.

“Diadora ni brand kubwa duniani na jezi zake zimewahi kuvaliwa na klabu kubwa duniani kama AS Roma na Simba inaendelea kukua ndio maana tumeamua kuvaa brand kubwa kama hii. Tutawapa ushirikiano wa kutosha na tunamuomba Mungu kuendelea kushirikiana nao kwenye maslahi ya pande zote mbili.” Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu.

Msafara wa klabu ya Simba Sc upo nchini Afrika ya kusini kwa ajili ya mchezo wa pili wa kombe la shirikisho dhidi ya Fc Stelleboch utakaofanyika kesho jumapili April 27 2025.

 

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited