Connect with us

Soka

Chama,Inonga Kuwakosa Namungo Fc

Klabu ya Simba sc itawakosa mastaa wake Cletous Chama na Henock Inonga sambamba na mastaa wengine kama Saido Ntibanzokiza,Luis Miqquisone na Shomari Kapombe kutokana na majeraha katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc utakaofanyika katika uwanja wa Majaliwa wilayani Ruangwa.

Sambamba na hao pia Mzamiru Yassin nae atakosekana kutokana na kuwa na kadi tatu za njano ambapo ataungana na Aishi Manula na John Bocco ambao ni majeruhi wa muda mrefu huku kocha Juma Mgunda sambamba na Seleman Matola wakitarajiwa kuongoza jahazi la klabu hiyo baada ya kocha Abdelhack Benchika kutimuliwa.

“Itakua mchezo mgumu maana Namungo ni Timu imara na ina wachezaji wazoefu kwa hiyo tunategemea kupata ushindani mkubwa lakini tumejidhatiti kwa ajili ya kupata ushindi”Alisema kocha wa klabu hiyo Selemani Matola akizungumza na waandishi wa habari.

Simba sc inapaswa kushinda mchezo huo ili kufufua matumaini ya kumaliza katika nafasi ya pili ama kutwaa ubingwa kutokana kuwa na michezo mitatu nyuma tofauti na Yanga sc na Azam Fc ambao wana michezo 24 huku Yanga sc akiwa kileleni na alama 62 na Azam Fc katika nafasi ya pili na alama 54.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka