Connect with us

Soka

Hersi Aitamani World Cup

Rais wa Yanga, Hersi Said amesema malengo ya timu hiyo ni kuhakikisha inakuwa moja ya klabu bora barani Afrika huku yeye binfasi akitamani kuona mwakani wakiingia kwenye timu nne bora Afrika ili waweze kushiriki Kombe la Dunia kwa ngazi ya klabu.

Hersi ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la vilabu barani Afrika (ACA) alisema hayo wakati akifanya mahojiano na kipindi cha bao la asubuhi ambacho kinaruka na Radio ya Bongo Fm ambapo alielezea matamanio yake hayo.

“Na matamanio yangu ni kuona mwakani kwenye mashindano ya Kimataifa tufike katika orodha ya timu nne bora Afrika, ili tuweze kushiriki Kombe la Dunia la Vilabu. Mwaka jana tumefika fainali na tumepata alama nyingi ambazo zitatuongezea nguvu ya kushiriki Kombe hilo” amesema Hersi Said.

Tangu achaguliwe kuwa Rais wa Yanga sc Hersi amefanya makubwa klabuni hapo ambapo pamoja na kutengeneza mfumo imara wa uongozi pia amefanikiwa kusajili mastaa wa maana na kuipa klabu makombe ya ligi kuu na kombe la shirikisho mara mbili mfululizo huku akifika fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka