Connect with us

Soka

Kambole Aiweka Matatani Yanga sc

Klabu ya Yanga sc imefungiwa kufanya usajili wa wachezaji wa ndani na Shirikisho la soka duniani (Fifa) kutokana na kutokamilisha malipo ya mshambuliaji Lazarus Kambole ambaye alishinda kesi dhidi ya klabu hiyo akidai malimbikizo ya malipo ya mishahara na pesa za usajili.

Kambole aliyejiunga na Yanga sc Juni 16 2022 na Septemba mwaka huo huo mshambuliaji huyo aliumia na kutolewa kwa mkopo kwenda klabu ya Wakiso Giant ya nchini Uganda ambapo alikaa kwa muda kabla ya klabu hiyo kumvunjia mkataba.

Kwa mujibu wa Taarifa kwa Umma iliyotolewa na Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF),Yanga sc ilipewa siku 45 za kumalizana na mchezaji huyo lakini imeshindwa kukamilisha malipo hayo na sasa imefungiwa kusajili kimataifa na TFF pia imeamua kuwafungia kufanya usajili wa ndani.

Hii si mara ya kwanza kwa Yanga sc kufungiwa kwani tayari ilikua imeshafungiwa na Fifa kutokana na kukiuka kipengele cha Annexe 3 ya kanuni ya usajili wa kimataifa ambapo kuna fomu ya malipo ya usajili ya mchezaji haijakamilika na hivyo kufungiwa na Fifa.

Pia klabu hiyo iliwahi kufungiwa kisa kutowalipa wachezaji kama Gael Bigirimana na kocha Luc Eymael kwa nyakati tofauti baada ya kuvunja nao mikataba bila kufuata utaratibu maalumu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka