Connect with us

Makala

Azam Fc Kukipiga na Wydad

Klabu ya Azam Fc usiku wa leo itaingia uwanjani katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco mchezo utakaofanyika katika mji wa Benslimane nchini humo ikiwa ni mchezo wa kwanza mgumu kwa Azam Fc.

Azam Fc ambao juzi kulazimishwa sare ya 1-1 na Union Touarga,watakua na kazi ngumu ya kukabiliana na Wydad ya Rulani Mokwena ambaye alikua kocha wa Mamelod Sundowns ya nchini Afrika ya kusini kabla ya kutimuliwa kutokana na matokeo mabaya ya mabingwa hao.

Wydad ambao ni  mabingwa wa zamani wa Morocco na Afrika wanauchukulia mchezo huo kama kipimo kizuri cha mastaa wake kuelekea msimu mpya wa ligi kuu ya nchini humo sambamba na michuano ya kimataifa.

Azam Fc baada ya mchezo huo watakwenda jijini Kigali kucheza na Rayon Sports katika siku ya Rayon Day kisha watarejea nchini kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya kwanza ya ngao ya jamii dhidi ya Coastal Union siku ya Augusti nane katika uwanja wa Amani Visiwani Zanzibar.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala