Connect with us

Masumbwi

Simba sc Yaangusha Alama Lindi

Klabu ya Simba sc imelazimishwa sare ya 2-2 na Namungo Fc katika mchezo wa ligi kuu nchini uliofanyika katika uwanja wa Ilulu mkoani Lindi jioni ya leo.

Simba sc ambayo iliwakosa mastaa Cletous Chama,Benard Morrison,Chris Mugalu na Hassan Dilunga kutokana na majeraha ilifungwa bao la mapema kwa kona na Jacob Massawe aliyefunga kwa kichwa dakika ya nane ya mchezo huku Simba sc waliamua kushambulia na kufanikiwa kupata bao kupitia kwa Meddie Kagere lakini mwamuzi alikaa akisema mfungaji alikua ameotea.

Shomari Kapombe aliisawazishia Simba sc dakika ya 42 ya mchezo na kufanya timu zote kwenda mapumziko zikiwa na sare ya 1-1 japo mapema kipindi cha Pili Obrey Chirwa alifunga bao la pili ambalo nalo halikudumu likasawazishwa dakika ya 78 na Kibu Dennis.

Simba sc sasa imefikisha alama 43 ikiachwa alama 12 na vinara wa ligi Yanga sc ambao wanahitaji kushinda jumla ya mechi tano tu katika ya 9 zilizobaki ili kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Masumbwi