Connect with us

Masumbwi

Mandonga Amtaka Dullah Mbabe

Bondia Karim Mandonga “Mtu Kazi” sasa amehamishia hasira zake kwa bondia Dullah Mbabe akitaka kupambana nae baada ya kutokea kujibizana kwa maneno baina yao.

Mandonga ambaye amekua maarufu nchini kutokana na kuwa na maneno ya shombo huku akipoteza mapambano licha ya kupewa kipaumbele kutokana na mikwara yake na maneno ya vitisho.

Mara ya mwisho bondia huyo alipigwa kwa Knock Out na Shabani Kaoneka katika pambano lililofanyika mjini Songea mkoani Ruvuma katika raundi ya nne tu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Masumbwi