Connect with us

Makala

Simba Sc Yatinga Fainali Cafcc

Klabu ya Simba Sc imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kupata suluhu katika mchezo wa marudiano dhidi ya Stelleboch Fc ya nchini Afrika ya kusini.

Katika mchezo wa awali Visiwani Zanzibar Simba sc iliibuka na ushindi wa 1-0 na kutanguliza mguu mmoja fainali ambapo jumapili ya Aprili 27 2025 walikua na kazi ya kulinda ushindi huo jambo ambalo lilitimia.

Simba sc ilianza mchezo huo kwa kasi lakini baada ya dakika 15 ilipoa na kuruhusu kushambuliwa mara kwa mara huku VAR ikiwaokoa Stelleboch baada ya mwamuzi kuamuru penati kwa Simba sc baada ya Kibu Dennis kuangushwa kipindi cha kwanza ndani ya eneo la hatari lakini penati hiyo iliyeyuka kufuati marejeo ya VAR.

Kipindi cha pili VAR iliwaokoa Simba sc baada ya mwamuzi kuamuru penati baada ya beki wa Simba sc kuunawa mpira lakini VAR ilionyesha kuwa haikua penati huku pia ikikataa goli ya Stelleboch baada ya mwamuzi kurejea na kuona kuwa kulikua na mtego wa kuotea.

Dakika tisini zilimalizika kwa Simba sc kushangilia uwanja mzima baada ya kufuzu fainali na sasa watamenyana na Rs Berkane ya nchini Morocco.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala