Connect with us

Makala

Azam Fc Apigwa Bao 1-0 Moro

Katika mchezo wa ligi kuu bara leo uliochezwa mkoani Morogoro uwanja wa Gairo umewapandisha nafasi ya 13 Mtibwa Sugar wakiwa na pointi 41 baada ya kuwafunga Azam Fc bao 1-0.

Bao hilo la kona lilifungwa na beki wa kushoto wa Mtibwa Sugar ,Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ dakika ya 37.

Mtibwa Sugar wameweza kulilinda bao hilo la pekee hadi dakika 90 za mchezo zilipotimilika kwani walifanyiwa mashambulizi mengi ya hatari ila umahiri wao wa ulinzi ukiongozwa na kipa chipukizi, Aboutwalib Mshery ndio uliyowafanya kunyakua alama tatu dhidi ya Azam Fc.

Azam Fc baada ya kupoteza mchezo huu wa leo wamebaki nafasi ya pili katika mchezo wa 35 wakiwa na pointi 65.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala