Connect with us

Makala

Zamalek Fc Yachukua Alama Tatu za Bure

Klabu ya soka ya Zamaleck Fc ya nchini Misri imefanikiwa kuchukua alama tatu na mabao mawili katika mchezo wa ligi kuu ya nchini Misri baada ya wapinzani wao klabu ya Al Ahly Fc kujitokeza uwanjani.

Awali mapema kabisa Klabu ya Al Ahly  Fc ilitangaza kugomea mchezo huo dhidi ya watani zao hao wa jadi kutokana na chama cha soka nchini humo kuamua kuwatumia marefa wa ndani badala ya wale wa kigeni.

Awali mwanzoni mwa msimu timu hizo zilikubaliana kuwa michezo ya ligi kuu baina ya mahasimu hao itachezeshwa na marefa kutoka nje ya nchi ili kuepusha upendeleo.

Hata hivyo kuelekea mchezo huo chama cha soka nchini humo kiliwateua waamuzi wa ndani kuchezesha mchezo huo hali iliyowafanya Al ahly kugomea mchezo huo.

Baada ya muda wa mechi kufika na Zamaleck kujipanga waamuzi walisubiria mpaka dakika ishirini za kikanuni kuona kama wapinzani watajitokeza na ndipo walipomaliza mpira na kuwapa ushindi wa mezani zamaleck.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala