Connect with us

Makala

Fadlu Achukua Tuzo ya Machi 2025

Kocha wa Simba Fadlu Davids amechaguliwa kuwa Kocha bora wa mwezi Machi wa Ligi kuu ya soka ya Nbc nchini akiwashinda kocha wa Azam Fc Rachid Taoussi Pamoja na kocha David Ouma wa klabu ya Singida Black Stars.

Fadlu ambaye ni raia wa Afrika ya kusini aliiongoza Simba kushinda mechi mbili ambapo waliifunga 6-0 Dodoma Jiji na kisha akawafunga mabao n3-0 klabu ya Coastal union na kuzoa alama zote sita katika mwezi huo.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa na Bodi ya ligi kuu nchini Tanzania imesema kuwa kocha huyo alionyesha ubora mkubwa katika ligi kuu kwa kupenyeza mbinu hizo kali ziliifanya klabu hiyo kuchukua alama zote.

Mpaka sasa katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini Simba sc ipo katika nafasi ya pili ikiwa na alama 57 ikicheza michezo 23 ya ligi kuu nchini huku Yanga sc akiwa kileleni akiwa na alama 67 katika michezo 26 ya ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala