Connect with us

Makala

Mukwala Atwaa Tuzo Machi 2025

Mshambuliaji wa klabu ya Simba sc Stephen Desse Mukwala amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Nbc kwa mwezi machi akiwashinda Ellie Mpanzu na Pascal Msindo wa klabu ya Azam Fc ambao aliingia nao Fainali.

Kamati ya Tuzo iliyochini ya bodi ya ligi kuu ilimchagua Mukwala kutokana na kuonyesha kiwango kizuri akifunga mabao manne katika mwezi huo ikiwemo kufunga mabao matatu katika mchezo mmoja (Hattrick) dhidi ya Coastal Union jijini Arusha katika uwanja wa Sheikh amri Abeid Kaluta.

Mukwala ambaye alianza kwa kususua katika miezi ya mwanzo ya ligi kuu,siku za hivi karibuni amefanikiwa kukuza kiwango chake na kuwa na uhakika wan amba katika klabu hiyo na mara nyingine akimuweka benchi mshambuliaji Lionel Ateba.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala