Connect with us

Soka

Chelsea,Liverpool hakuna mbabe

Mechi iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka duniani baina ya Chelsea na Liverpool imeshindwa kupata mbabe baada ya timu hizo kutoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.

Liverpool ndio waliokuwa wa kwanza kupata mabao yote mawili kupitia kwa Sadio Mane dakika 9 ya na Mohamed Salah dakika ya 26,kabla ya wenyeji kurejea mchezoni na kusawazisha kupitia Mateo Kovacic dakika ya 42 na Christian Pulisic dakika ya 45+1.

Katika mchezo huyo Liverpool ilimkosa kocha wake mkuu Jurgen Klopp kutokana na maambukizi ya Uviko-19 pamoja na wachezaji Thiago Alcantara,Alison Becker na Joel Matip,huku Chelsea ikiwakosa Andres Christensen na Timo Werner kwa matatizo hayo hayo.

Sare hiyo imepelekea mbio za ubingwa wa ligi kuu soka nchini Uingereza kubaki za upande mmoja baada ya tofauti ya pointi kati ya vinara Manchester city na anayeshika nafasi ya pili Chelsea kuwa ni alama kumi baada ya michezo 21.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka