Connect with us

Masumbwi

Kidunda kulipa kisasi kwa Katompa

Bondia kutoka Jeshi la Wananchi Suleiman Kidunda atapanda ulingoni Christmas hii kupambana na Mkongomani Tshimanga Katompa katika pambano lililopewa jina la ‘Boxing on Boxing Day’ litakalofanyika siku ya Boxing day katika ukumbi wa Ubungo Plaza Jijini Dar es salaam.

Pambano hilo ambalo awali liliota mbawa ni la kulipiza kisasi kwa bondia Dulla Mbabe aliyepigwa na Katompa katikati ya mwaka huu,kitu ambacho kiliwasikitisha Watanzania waliotaka Katompa arudi tena Tanzania ili walipize kisasi.

Baada ya pambano la Dulla Mbabe na Katompa,Kidunda alipost katika mtandao wake wa Instagram kuwa yeye anataka apambane na Katompa kwani kupigwa kwa Dulla ni kuliaisha Taifa.

Mapambano mengine yanatarajiwa kufanyika siku hiyo ni pamoja na

Ibrahim Classic vs Kamenda (Malawi)

Ismail Galiatano vs Denis (Malawi)

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Masumbwi