Connect with us

Makala

Ibrahim Class Amtwanga Mchina

Bondia Mtanzania Ibrahim Class ameshinda pambano la ubingwa wa TPBRC dhidi ya bondia raia wa China Xiao Tau Su katika pambano hilo la ubingwa wa Afrika lililofanyika katika ukumbi wa PTA sabasaba jijini Dar es salaam.

Pambano hilo ambalo ndio lilikua pambano kuu katika usiku huo ambapo katika mapambano ya utangulizi bondia Fadhil Majiha alifanikiwa kumpiga bondia kutoka Afrika ya kusini Bongani Mahlangu katika pambano la raundi 10 na kufanikiwa kupata mkanda wa ubingwa wa WBC (World Boxing Council).

Katika pambano hilo kuu Ibrahim Class ilimlazimu afanye kazi ya ziada kumthibiti Tau Su ambaye naye alikua moto kwa kupeleka ngumi za haraka haraka huku akitumia akili zaidi katika kujilinda.

Uamuzi wa majaji baada ya raundi ya mwisho ndio uliompa ushindi Class kwa pointi huku akithibitisha ubora wa mpinzani wake huyo wakati wa mahojiano.

Mimi ni mwanaume na siyo mvulana”alisema Ibrahim Class wakati akiongea na waandishi ambapo alisema kuwa kama sio uimara na uzoefu wake basi angepoteza pambano hilo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala