Connect with us

Masumbwi

Bondia Mtanzania Fadhili Majiha ‘Kiepe Nyani’ ambaye ni bingwa wa mkanda wa WBC Afrika ameweka rekodi ya kuwa Bondia wa kwanza nchini kupata hadhi ya nyota nne na nusu akivunja rekodi ya  mabondia Hassan Mwanyiko na Tony Rashid katika Mtandao wa maalumu wa Takwimu za mabondia wa Boxrec.

Bondia huyo amefikia kiwango hicho wiki moja baada ya kushinda kwa pointi dhidi ya mpinzani wake  Bongani Mahlangu wa Afrika Kusini katika pambano la Raundi 10 lililoffanyika katika ukumbu wa sabasaba wilayani Temeke.

Pamoja na kufikisha hadhi hiyo Pia ameingia kwenye orodha ya Mabondia 10 Bora Duniani uzani wa Bantam, akishika nafasi ya 7 kati ya 1,056.

Mwakinyo ndiye Bondia wa kwanza Nchini kufikia Hadhi ya Nyota 4 lakini kwa sasa ameshuka mpaka nyota 2 katika uzani wa Super Walter wakati Tony Rashid ana Nyota 2.5 katika Uzani wa Super Bantam.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Masumbwi

 • Mwakinyo Huru

  Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBRC) imemfungulia bondia Hassan Mwakinyo kutoka kifungoni baada...

 • Ibrahim Class Amtwanga Mchina

  Bondia Mtanzania Ibrahim Class ameshinda pambano la ubingwa wa TPBRC dhidi ya bondia raia...

 • Mwakinyo Aitwa Mahakamani

  Kampuni ya PAF Promotion imemfungulia shauri la madai Bondia Hassan Mwakinyo ambalo linatarajiwa kutajwa...

 • Mwakinyo Afungiwa Mwaka 1

  Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania Hassan Mwakinyo amefungiwa mwaka mmoja kushiriki mapambano...