Connect with us

Makala

Winga Mkenya Anukia Msimbazi

Klabu ya Simba sc ipo mbioni kukamilisha usajili wa winga raia wa Kenya Harrison Mwenda ambaye tayari amewasili nchini asubuhi ya leo kukamilisha taratibu za mwisho kumwaga wino katika klabu hiyo ambao wapo nafasi ya pili katika ligi kuu nchini.

Mwenda mpaka sasa alikua akiitumia klabu ya Kabwe Warriors inayoshiriki ligi kuu nchini Zambia na endapo atashindwana na Simba sc basi anaweza kuelekea nchini Afrika ya kusini ambako pia amepata ofa kadhaa.

Winga huyo anayetumia mguu wa kushoto aliwahi kutamba na timu za Mathare United, Kariobangi Sharks na AFC Leopards amekuwa akiwindwa na Simba tangu kwenye dirisha dogo la usajil la msimu lakini dili lake lilikwama kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala