Connect with us

Makala

Geita Gold Fc Wakumbwa na Rungu la Fifa

Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA limeifungia Klabu ya Geita Gold kutosajiri Mchezaji yeyote Mpaka pale itakapolipa Madai ya mishahara ya aliyekuwa Kocha wao Etienne Ndayiragije.

Geita Gold ilivunja mkataba na Ndayiragije baada ya kutoridhishwa na matokeo ya timu kwenye michezo yake ya awali mwanzoni wa Msimu huu na kuamua kumrejesha kocha Fred Felix Minziro ambaye aliipandisha timu hiyo daraja.

Kutokana na suala hilo inasemekana kwamba klabu hiyo haikukamilisha baadhi ya stahiki za kimkataba na kumfanya kocha huyo kukimbilia katika shirikisho hilo la soka duniani kudai haki zake na ndipo Fifa ilipojiridhisha imeamua kutoa hukumu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala