Connect with us

Makala

Stars Yapoteza Kwa Morocco

Timu ya soka ya Wanaume ya Tanzania (Taifa Stars) imepoteza mchezo wa kuwania kufuzu kombe la dunia mwaka 2026 dhidi ya Morocco baada ya kukubali kufungwa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika nchini humo.

Stars pamoja na kujitahidi kupambana lakini ilizidiwa uwezo na wenyeji ambapo mpaka kipindi cha kwanza matokeo yalisalia 0-0 licha ya kocha Hemed Morocco kumuanzisha kipa mgeni Yakub Selemani Ali wa Jkt Tanzania.

Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Manispaa nchini humo ulishuhudia Nayef Arguerd akifunga bao la kwanza dakika ya 51 kisha Brahim Diaz alifunga kwa penati dakika ya 58.

Sasa Morocco ni rasmi wamefuzu kushiriki kombe la dunia mwaka 2026 katika nchi za Mexico,Canada na Marekani baada ya kukusanya alama 15 kileleni mwa kundi E ikishinda michezo yote mitano huku Tanzania ikiwa nafasi ya tatu na alama sita sawa na Niger walionafasi ya pili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala