Connect with us

Makala

Yanga Sc Yamfukuzia Silla Kimya Kimya

Mabosi wa klabu ya Yanga sc wamevutiwa na uwezo wa winga wa Azam Fc Gibril Sillah ambaye mkataba wake uko mbioni kumalizika katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Yanga sc inafanya ushawishi wa kimyakimya kuhakikisha inampata Djibril Sillah, Winga wa Azam mwisho wa msimu huu ikitaka dili hilo limalizike kwa haraka kabla ya ligi kumalizika.

Sillah Mkataba wake unafika ukingoni mwisho wa msimu huu mpaka sasa hajassini mkataba mpya katika klabu hiyo huku mazungumzo baina yake na mabosi wa Azam Fc yakiwa bado hawajafikia muafaka.

Yanga wanahitaji Winga anayetumia mguu wa kushoto na wanaona winga huyo aliyewafunga mara kadhaa kuwa anafaa kuchukua nafasi hiyo.

Kazi kubwa inafanyika kumtengea dau la maana staa huyo ili kumshawishi kutua jangwani japo mabosi wa klabu yake ya sasa wanapambana kumbakisha.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala