Connect with us

Makala

Rs Berkane Wakimbilia Caf

Klabu ya RS Berkane ya Morocco imewasilisha malalamiko kwa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuhusu mwamuzi wa DR Congo, Jacques Ndala Chuma alicheyezesha mchezo dhidi ya Simba SC na kutaka afungiwe.
Berkane wanadai Ndala alihongwa ndio maana aliwanyima penati kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam huku
Pia wakisema walipata bao la wazi lakini walinyimwa kwa sababu mchezaji wao alikuwa tayari ameshaotea (offside).
Wamorocco hao pia wanadai Simba sc ilipoteza muda mwingi na mwamuzi wa akiba akaongeza dakika nne tu za kuchezwa ambapo wengi walitarajia kungeongezwa zaidi ya dakika tano na kuendelea kutokana na uwepo wa matukio yaliyosababisha mpira kusimama.
Klabu hiyo inaitaka CAF kumuadhibu mwamuzi na wasaidizi wake wote kwa kufungiwa ikiwezekana kwa kushindwa kutenda haki katika mchezo huo uliomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala