Connect with us

Makala

Simba Sc Yamalizana na Kibu

Sasa ni rasmi kwa mshambuliaji wa klabu ya Simba sc Kibu Dennis amesaini mkataba wa miaka miwili kutumia klabuni hapo baada ya kukubaliana na mabosi wa klabu hiyo baada ya mvutano wa muda mrefu baina yao na kuzima tetesi za kuhitajika na klabu za Yanga sc,Azam Fc na Ihefu Fc.

Kibu amesaini mkataba huo wenye maboresho makubwa ya mshahara na dau la usajili huku akipata bonasi za uhakika ambapo timu yake itashinda na kumfanya kwa mwezi kufikisha takribani milioni 15 ikijumuisha mshahara na marupurupu mengine ya kimkataba huku akipokea dau la usajili linalokadiriwa kuwa kiasi cha shilingi milioni mia tatu ambapo atalipwa kwa awamu mbili huku akipewa gari la shilingi milioni 50 za kitanzania.

Simba sc imepambana mpaka kuipata saini ya mshambuliaji huyo ambayo licha ya takwimu kuonyesha kuwa amefunga bao moja pekee katika michezo 20 lakini uwezo wake wa kupambana uwanjani ambayo ni moja ya jambo linalowafanya waalimu wengi kumtumia uwanjani.

Simba sc ilimsajili Kibu misimu miwili iliyopita akitokea Mbeya Fc kwa mkataba wa miaka miwili kwa dau linalofikiwa milioni mia mbili ambapo ilizishinda baadhi ya klabu ambazo zilikua zinamnyemelea hapa nchini ikiwemo Azam Fc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala