Connect with us

Makala

Chama Atemwa Chipolopolo

Kocha wa timu ya Taifa ya Zambia Avram Grant ameamua kumtema kiungo wa klabu ya Simba sc Cletous Chama katika kikosi cha wachezaji watakaojiunga na kambi ya timu hiyo kujiandaa na michezo ya kimataifa dhidi ya Tanzania na Morroco.

Kikosi cha wachezaji 27 kimeitwa kwa ajili ya michezo miwili ya Juni 7 na 11 kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia mwaka 2026 zitakazofanyika mwaka 2026 katika nchi za Canada,Mexico na Marekani.

Kocha Grant pamoja na kumtema Chama pia amemujumuisha mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Kennedy Musonda katika kikosi hicho ambapo ataungana na washambuliaji Patson Daka,Evance Kangwa,Kingston Mutandwa na Edward Chilufya.

Wachezaji wengine walioitwa kikosini ni makipa Lawrence Mulenga,Victor Chabu,Toaster Nsabata na upande wa mabeki ni Stoppilla Sunzu,Tandi Mwape,Chongo Kabaso,Killian Kanguluma,Frank Musonda,Gift Mphande na Luka Banda.

Viungo ni pamoja na Benson Sakala,Miguel Chaiwa,Obina Chisala,Lubambo Musonda,Abraham Siankombo,Kelvin Kampumbu,Emmanuel Kombo,Joshua Mutale,Kings Kangwa,Kelvin Kampamba na Gamphan Lungu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala