Connect with us

Makala

Pumzi ya Moto

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Rs Berkane katika mchezo hatua ya makundi ya michuano shirikisho barani Afrika uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba sc ikianza na mshambuliaji Meddie Kagere na Kibu Dennis ililazimika kusubiri mpaka mwishoni mwa kipindi cha kwanza kupata bao ambapo juhudi binafsi za Pape Osmane Sakho zilizaa matunda na kuweza kuipa uongozi klabu yake baada ya kuingia kwenye boksi na kuwalaghai mabeki wa Berkane na kufanikiwa kufunga kwa shuti kali.

Kipindi cha pili licha ya juhudi za Simba sc kusaka bao la pili lakini ilishindikana huku wakikosa mabao ya wazi kupitia kwa Bernad Morrison huku pia refa akiwanyima iliotafsiriwa kuwa penati na wachezajin wa berkane baada ya kipa Aishi Manula kugusa mguu wa mshambuliaji wa Rs Berkane lakini mwamuzi aliamuru ipigwe kona hali iliyoamsha hasira za wachezaji na viongozi wa Rs Berkane.

Kipigo hicho kinamuweka matatani kocha Frolent Ibenge ambaye uongozi wa klabu ya Rs Berkane unamfuatilia kwa ukaribu kuona maendeleo yake baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo licha kuwafunga Simba sc mabao 2-0 katika mchezo wa awali nchini Morocco.

Simba sc sasa imefikisha alama 7 ikiwa inaongoza kundi hilo huku Rs Berkane na Asec Mimosa wakiwa nafasi ya pili na tatu kwa alama 6 huku Us Gendamarie wakishika mkia.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala