Connect with us

Makala

Morrison Majanga Tupu

Winga machachari wa klabu ya Simba sc Mghana Benard Morrison alikamatwa na polisi baada ya mchezo dhidi ya Yanga sc uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Iko hivi wakati timu zikiondoka staa huyo hakupanda basi la timu na aliondoka na gari yake binafsi lakini mashabiki walimzonga wakimzomea na kumtania kitu kilichomkera staa huyo na kuamua kuchukua kitu chenye ncha kali na kumshambulia mmoja wa mashabiki hao ambaye aliumia na kuvuja damu jambo lililowalazimu Polisi wa kituo cha Chang’ombe kumkamata kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani tayari mchezaji huyo ameshaachiwa na Polisi na jana alishiriki mazoezi kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo FC utakaofanyika mkoani Lindi katika uwanja wa Ilulu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala