Connect with us

Makala

Yanga sc Yaifuata Ruvu Kigoma

Kikosi cha klabu ya Yanga sc kimeondoka asubuhi ya leo kuelekea Kigoma kuvaana na Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu utakaofanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika uliopo mjini Kigoma.

Mchezo huo umepelekwa mkoano humo na wenyeji wa mchezo huo ambao ni Ruvu Shooting ambapo timu mwenyeji anaruhusiwa kuchagua uwanja atakaojisikia tofauti na ule wa nyumbani katika mechi mbili za msimu mmoja  kwa mujibu wa Kanuni za ligi kuu nchini.

Mastaa Feisal Salum,Djuma Shabani,Fareed Mussa,Yannick Bangala,Jesus Moloko walionekana wakiwa uwanja wa ndege kueleka mkoani humo kusaka alama tatu muhimu katika kuhitimisha mbio za ubingwa wa ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala