Connect with us

Makala

Ronaldo Aikoa Man Utd

Cristiano Ronaldo amefanikiwa kuikoa klabu ya Man utd na kipigo baada ya kusawazisha bao dakika ya 62 na kuifanya Man united iambulie sare katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Chelsea uliofanyika katika uwanja wa Old Trafford jijini Manchester.

Marcos Alonso aliifungia Chelsea bao lililodumu kwa dakika mbili na kusawazishwa na Ronaldo dakika ya 62 akipokea pasi kutoka kwa kiungo Nemanja Matic huku wageni wakiukamata mchezo kwa kushambulia kwa kasi japo walikosa nafasi nyingi za wazi.

Usajili wa Ronaldo umeendelea kuwalipa Man United ambapo mpaka sasa amefunga mabao 17 huku katika mabao tisa ya klabu hiyo katika ligi kuu nchini Uingereza staa huyo amefunga mabao 8 peke yake na kumfanya kuwa mchezaji muhimu klabuni hapo.

Man united sasa wanafikisha alama 55 katika michezo 35 wakiwa nafasi ya sita ya msimamo huku Chelsea wakiwa nafasi ya tatu na alama 66 katika michezo 33 ya ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala