Connect with us

Makala

Masoud Djuma,Mtegete wala Kibano

Kocha wa timu ya Dodoma Jiji Fc Masoud Djuma na mchezaji wa klabu hiyo Jamal Mtegeta wamefungiwa na bodi ya ligi kwa kosa la kupigana wakati wa mchezo ambapo adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 45;5(2.1) inayohusu udhibiti wa makocha na kanuni 41:5(5.1) inayohusu udhibiti wa wachezaji.

Kwa mujibu wa bodi ya ligi kuu nchini imesema kuwa kocha huyo alimpiga teke mchezaji huyo wakati wa mchezo wa ligi kuu namba 173 kati ya Biashara united na Dodoma jiji ambapo baada ya mchezaji kupigwa teke na kocha huyo nae aliamua kumrudishia na ndipo purukushani zilipoanzia kiasi cha kusababisha utulivu kukosekana katika eneo la wachezaji wa akiba la timu hiyo.

Pamoja na adhabu hiyo ya kufungiwa michezo mitatu kila mmoja pia watawajibika kulipa faini ya kiasi cha shilingi laki tano za kitanzania kila mmoja.

Pia pamoja na adhabu hiyo kwa wachezaji na kocha pia kipa wa klabu hiyo pamoja na kipa wa klabu ya Polisi Tanzania wamepewa onyo kali kwa kosa la kuvaa soksi zenye rangi tofauti na zile zilizokubaliwa wakati wa kikao cha maandalizi ya mchezo hali iliyosababisha mchezo kuchelewa kwa dakika 10 kuwasubiri wakabadilishe katika mchezo namba 177 uliowakutanisha klabu ya Polisi Tanzania dhidi ya Dodoma Jiji.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala