Connect with us

Makala

Mpole Amfunika Mayele

George Mpole wa Geita Gold Fc amekaa juu ya kilele cha mfungaji bora wa ligi kuu ya Nbc nchini baada ya kufikisha mabao 13 na kumpita staa wa Yanga sc Fiston Mayele mwenye mabao 12 ya ligi kuu nchini.

Mpole amekaa kileleni hivi leo baada ya kufunga bao la 13 katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya Kwanza Fc uliofanyika katika uwanja wa Majimaji mjini Songea ambapo alifunga bao hilo dakika ya 11 ya mchezo baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Mbeya kwanza na mpira kumkuta Mpole aliyefunga kwa shuti kali.

Mbeya kwanza licha ya juhudi za kutaka kusawazisha walijikuta wakilazimika kucheza pungufu kufuatia mchezaji wake Enock Jiah kupata kadi ya pili ya njano dakika ya 74 ya mchezo na kufifisha jumla matumaini ya timu hiyo kusawazisha bao hilo ambalo lilidumu mpaka dakika 90 za mchezo.

Kutokana na matokeo hayo sasa Geita Gold Fc wamepanda mpaka nafasi ya tatu wakiwa na alama 34 huku Mbeya kwanza wakibaki mkiani mwa ligi kuu wakiwa na alama 23 na kuendelea kuwa katika hatari ya kushuka daraja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala