Connect with us

Makala

Simba sc Yamponza Kocha Orlando Pirates

Kocha mkuu wa klabu ya Orlando Pirates Mandla Ncikazi amepewa barua ya onyo na shirikisho la soka barani Afrika (Caf) kufuatia kauli alizozitoa kwa waandishi wa habari baada ya mchezo wa raundi ya kwanza ya robo fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya Simba sc uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Baada ya mchezo huo uliomalizika kwa Simba sc kushinda kwa penati 1-0 kocha huyo alilalamikia kuhusu mapokezi ya Simba sc kuwa yalikua mabovu na hasa ndio sababu kubwa ya kufungwa kwa timu yake pamoja na mazingira hafifu kabla ya mchezo waliyopewa na Simba sc.

Kufuatia tuhumu hizo Simba sc ilituma malalamiko Caf kuomba muongozo zaidi kufuatia kuchafuliwa na kocha huyo ilhali walifanya kila kitu kwa mujibu wa sheria za Caf na sasa shirikisho hilo limempa onyo kali kocha huyo ambaye timu yake imefuzu hatua ya fainali na itacheza na Rs Berkane ya nchini Morroco.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala