Connect with us

Makala

Mamilioni ya Samia Yatua AFL

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa zawadi ya Tsh.10 milioni kwa kila goli ambalo Simba sc  watafunga katika mchezo dhidi ya Al Ahly ambao utachezwa siku ya Ijumaa Oktoba 20, 2023 saa 12:00 jioni katika Uwanja wa Mkapa.

Ahadi hiyo ya Rais Samia imetolewa na katibu mkuu wa Wizara ya Michezo,Sanaa na Utamaduni Gerson Msigwa wakati akizungumza na waandishi wa habari mapema hivi leo jijini Dar es salaam wakati alipojiunga na kampeni ya kuhamasisha mashabiki wa klabu ya Simba sc kununua tiketi za mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo mipya.

“Nimeongea na Mh.Rais Samia Suluhu Hassan amesema nenda kawahamasishe wanasimba na watanzania wote kuwa mechi hii ni ya Watanzania lakini alisema japo hakua amesema kuwa nije niwaambie katika kila mechi ya michuano hii ya AFL ambayo Simba Sc watashinda basi kila goli moja atatoa shilingi milioni kumi”Alisema Msigwa ambaye alikua Msemaje wa serikali kabla ya kupewa cheo cha sasa cha ukatibu mkuu wa Wizara ya michezo

Simba sc itacheza na Al Ahly katika ufunguzi wa michuano hiyo mipya nchini siku ya Ijumaa huku ikitarajiwa kuwa na wageni wengi mashuhuri akiwemo Rais wa Fifa Gian Infantino.

Hamasa hii ya goli la mama ilianza msimu uliopita kwenye michuano ya kimataifa ambapo Simba na Yanga zilikuwa zikichuana kuchukua fedha hizi ikiwa msimu uliopita ilikuwa ni shilingi milioni 5 kila goli.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala