Connect with us

Makala

Bangala Kuikosa Yanga sc

Kiungo wa klabu ya Azam Fc Yannick Bangala Litombo anatarajiwa kuukosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga sc utakaofanyika siku ya Jumapili Oktoba 2 jijini Dar es salaam katika uwanja wa Chamazi kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya misuli.

Kiungo huyo aliyesajiliwa kutokea Yanga sc aliumia na kulazimika kutolewa nhe wakati wa suluhu dhidi ya Dodoma Jiji katika uwanja wa Jamhuri ambapo mpaka sasa bado hajarejea katika utimamu wake wa kawaida.

Azam Fc itakua na mtihani mzito kuhakikisha inaongeza pengo kwa alama tatu zaidi dhidi ya Yanga sc ambayo imezidi kwa alama moja ikiwa na alama 13 huku Yanga sc ikiwa na alama 12 katika nafasi ya tatu ya msimamo.

Afisa Habari wa timu hiyo, Hashim Ibwe amesema kuwa mbali na kiungo huyo pia kuna na beki wa kati, Abdallah Kheir ‘Sebo’ ambaye alifanyiwa oparesheni ya goti.

“Bangala na Sebo ndio wachezaji pekee watakaokosekana katika mchezo wa Dar es salaam Dabi tutakaocheza dhidi ya Young Africans, lakini wachezaji wengine wote wapo fiti.

“Bangala alipata maumivu ya misuli katika mchezo wetu wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji, lakini hivi sasa anaendelea vizuri na upo uwezekano mkubwa wa kurejea haraka uwanjani baada ya kupata nafuu.

“Mchezo wetu huu ni muhimu kupata ushindi, kwa lengo la kulipa kisasi cha kufungwa katika nusu fainali ya Ngao ya Jamii, uzuri wachezaji wapo katika morali kubwa ya ushindi,” amesema Ibwe

Bangala amejiunga na Azam fc baada ya kuitumikia klabu ya Yanga sc kwa misimu miwili ambapo Yanga sc ilimuuza kwa dau la Shilingi milioni mia moja kwenda katika klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala