Connect with us

Makala

Al Hilal Kulipa Mamilioni Kushiriki Npl

Klabu ya Al Hilal ya Sudan itawalazimu kuingia mfukoni na kulipa mamilioni ya fedha kwa ajili ya kikosi cha wachezaji 38 pamoja na benchi la ufundi ili kupata idhini ya kucheza michezo ya Ligi Kuu Bara msimu ujao wa 2024-2025 ambapo mpaka sasa ombi lao liko mwishoni kukamilika.

Mabosi wa timu hiyo wametuma barua hapa nchini kwa Shirikisho la soka wakiomba kushiriki katika ligi kuu ya soka ya Nbc hapa nchini kwa lengo la kuendelea kupata mechi za ushindani kutokana na mzozo wa kisiasa unaondelea nchini Sudan.

Pamoja na kwamba bado Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linaendelea na vikao vyake juu ya namna nzuri ambayo wababe hao wa Sudan watashiriki Ligi Kuu Bara kwa kipindi kifupi kutokana na maombi hayo ambapo endapo watakubaliwa itawalizimu kulipa kiasi cha Tsh milioni 230 kwa mamlaka za Tanzania kutokana na wachezaji hao kutambulika kama wachezaji wa kigeni.

TFF imeweka utaratibu wa kila mchezaji wa kigeni kulipia kibali cha kupata leseni ya kucheza ligi kuu nchini ambapo mastaa hao wote hawana budi kulipiwa kupata kibali hicho ili kupata ridhaa ya kushiriki ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala