Connect with us

Makala

Kibabage Kutua Yanga sc

Uongozi wa Yanga upo kwenye mazungumzo ya kumsajili Nickson Kibabage akitokea Singida Fountain Gate alikodumu kwa msimu mmoja pekee baada ya kusajiliwa akitokea klabu ya Mtibwa Sugar ya Manungu mkoani Morogoro.

Yanga na Kibabage wamemalizana upande wa maslahi binafsi  na sasa kinachoendelea ni majadiliano ya dau la uhamisho kati ya Yanga na Singida Fountain Gates ambako bado ana mkataba.

Kibabage ana uwezo wa kucheza kama winga ama beki wa kushoto nafasi ambazo amekua akizicheza vizuri akiwa katika klabu za Difaa El Jadid ya nchini Morroco na hata alipojiunga na Mtibwa Sugar.

Usajili wa Kibabage kuja Yanga sc unakuja kuziba nafasi ya beki wa kushoto David Bryson ambaye anaweza kuachwa muda wowote kutokana na kushindwa kuendana na kasi ya Kibwana Shomari aliyehamishiwa upande huo na Joyce Lomalisa Mutambala.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala