Connect with us

Makala

Azam Fc Yawafunga Mastaa

Kuelekea msimu mpya wa ligi kuu na michuano ya kimataifa klabu ya soka ya Azam Fc imefanikiwa kuwasainisha mikataba mipya baadhi ya mastaa wa klabu hiyo kutokana na kuridhishwa na viwango vyao hivyo kuamua kuwalinda wasichukuliwe na klabu zingine.

Wengi wa mastaa hao walikua wamesalia na mikataba mifupi ya mwaka mmoja huku wengine kama Sospeter Bajana walikua wamemaliza mikataba yao.

Mastaa kama Prince Dube,Kipre Jr,Daniel Amoah,Nathanael Chilambo,James Akaminko wameongeza mikataba ambapo watakua klabuni hapo mpaka mwaka 2025.

Pamoja na kuwaongezea mikataba mastaa hao pia Azam Fc imewapa mikono ya kwaheri mkongwe Aggrey Morris,Wilboard Maseke,Kenneth Muguna,Rodgers Kola na Bruce Kangwa huku katika benchi la ufundi wakiachana na Dan Cadena na Kally Ongala.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala