Connect with us

Makala

Jezi Yanga sc Gumzo

Jezi ya klabu ya Yanga sc zimekua gumzo mjini tangu kuzinduliwa kwake siku ya jana ambapo wanachama na mashabiki wa klabu hiyo wamejaa kila kona kuziombania jezi hizo zenye rangi tatu tofauti.

Yanga sc wamezindua aina tatu za jezi kwa ajili ya msimu ujao ambazo zitakua za nyumbani,ugenini na aina ya tatu zenye rangi za kijani,njano na nyeusi ambazo zote zimebuniwa na mbunifu maarufu nchini Sheria Ngowi.

Jezi hizo zimebuniwa zikiwasilisha ujumbe tofauti tofauti ikiwemo inayoonyesha utalii wa ndani ambayo ina majengo na maeneo maarufu nchini ikiwemo Posta katikati ya mji,Daraja la Nyerere lililopo Kigamboni na vivutio vingine maarufu nchini ikiwemo mlima mrefu barani Afrika wa Kilimanjaro.

Zingine zimewasilisha muunganiko wa matawi ya wanachama wa klabu hiyo huku nyeusi ikiwasilisha historia ya klabu hiyo ambapo ina sahihi za wakongwe kama Sunday Manara,Abeid Mzimba,Mohamed Hussein,Edibily Lunyamila na wengineo.

Yanga sc tayari imeshaanza kusambaza jezi hizo ambazo zinapatikana katika maduka ya Gsm na katika makuu makuu ya klabu yaliyopo Jangwani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala