Connect with us

Makala

Simba Week Kuzinduliwa Mbagala J’pili

Klabu ya Simba sc imetangaza kuwa itafanya uzinduzi wa wiki ya Simba kuelekea katika kilele cha siku ya Simba day ambayo hufanyika kila mwaka August 8 siku ambayo huwa ni sikukuu ya wakulima nchini.

Mkuu wa Idara ya Habari ya klabu hiyo Ahmed Ally ametangaza kuwa uzinduzi wa wiki hiyo ya Simba sc utafanyika katika viwanja vya Mbagala Zakhiem siku ya Jumapili Julai 31 katika viwanja hivyo.

Simba sc imekua na utaratibu wa kuazimisha siku ya Simba day kila mwaka ambapo tamasha hilo maarufu nchini hutumika kutambulisha wachezaji wapya wa klabu hiyo pamoja na benchi la ufundi la klabu hiyo ambayo kwa sasa ipo nchini Misri kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu mpya.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala