Connect with us

Makala

Yanga sc Walamba Dili Nono

Klabu ya Yanga sc imesaini mkataba mnono wa udhamini na kampuni ya michezo ya kubashiri ya Sportspesa ambao una thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania Bilioni kumi na mbili na ushee kwa muda wa miaka mitatu.

Mkataba huo umesainiwa leo mbele ya waandishi wa habari katika hoteli ya Johari Rotana iliyopo katikati ya jiji ambapo klabu hiyo itajipatia kiasi cha Bilioni 4 na milioni kadhaa kwa mwaka kwa muda wote wa mkataba wa miaka mitatu,

Mbali na kiasi hicho klabu hiyo pia itajipatia bonansi za ziada za shilingi milioni 150 endapo itatatwaa taji la ligi kuu nchini huku pia itapata kiasi cha Shilingi milioni 75 endapo itafanikiwa kuingia nusu fainali ya kombe la shirikisho la Azam.

Awali klabu ya Yanga sc iliingia mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya kiasi cha Shilingi Bilioni 5 kwa muda wa miaka mitano ambapo kwa mwaka walikua wakipata bilioni moja pekee lakini mkataba huu mpya na kampuni hiyo imekua mkubwa kiasi cha wadau mbalimbali wa soka wameipongeza klabu hiyo kupata udhamini mkubwa wa fedha huku pia fedha hizo zikilipwa kila mwezi ili kusaidia uendeshaji wa klabu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala