Connect with us

Makala

Hapatoshi Simba sc Vs Mbeya City Fc

Klabu ya Simba sc imewasili nchini jana jioni tayari kwa mchezo wa ligi kuu nchini dhidi ya Mbeya City Fc utakaofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam jioni ya leo saa moja za usiku.

Simba sc inaingia na nguvu mpya ikitoka kumfunga Tanzania Prisons Fc 7-1 huku pia ikiwa na maingizo mapya kikosini wakiwemo Ismael Sawadogo,Jean Baleke na kinda Mohammed Musa aliyesajiliwa kutokea visiwani Zanzibar lakini pia inatarajiwa kukutana na upinzani mkali kutoka kwa Mbeya City yenye mastaa wa nguvu wakiwemo James Msuva,Salum Kihimbwa,AbdulRazack Hamza na Charles Masenga.

Mchezo unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa timu zote ili kuangalia usajili mpya wa vikosi hivyo jinsi utakavyoleta mabadiliko hasa kwa Simba sc ambaye imerejea kutoka katika kambi ya kujinoa jijini Dubai falme za kiarabu.

Simba sc mpaka sasa ina alama 44 ikicheza jumla ya michezo 19 katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu nchini huku Mbeya City Fc ikiwa katika nafasi ya 10 ikiwa na alama 21 katika michezo 19 ya ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala