Connect with us

Makala

Morrison,Yanga sc Kumekucha

Uhusiano baina ya klabu ya Yanga sc na mchezaji wake Benard Morrison unaelekea kuzorota baada ya staa huyo kuchelewa kuripoti kambini tangu alipokwenda nchini kwa Ghana kwa ruhusa maalumu ambapo amechelewa kurudi na kukosa mchezo mmoja wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc.

Taarifa za ndani zinadai kuwa staa huyo amechelewa makusudi akishinikiza kulipwa baadhi ya stahiki zake za usajili ambazo uongozi haujamlipa ambapo pia mastaa wengine kama Yannick Bangala na Khalid Aucho wamegomea pia japo taarifa hizo hazina uthibitisho rasmi.

Morrison anatajwa kama ni moja ya usajili mbovu katika klabu ya Yanga sc kutokana na kuwa na utovu wa nidhamu uliokithiri hasa kuchelewa kuripoti kambini ambapo kocha Nabi amekua mkali dhidi ya staa huyo huku akiwa amechangia upatikana wa mabao manne pekee mpaka sasa huku akikosa mechi kadhaa.

Afisa habari wa klabu ya Yanga sc alisikika akisema kuwa suala la Morrison litatolewa maelekezo na Afisa Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Andre Mtine ambapo sasa suala hilo linashughulikiwa kwa ukaribu zaidi.

Morrison alikua kipenzi cha mashabiki wa Yanga sc mpaka pale alipoamua kuachana na Yanga sc na kujiunga na Simba sc kwa mkataba wa miaka miwili katika usajili ambao ulikua na kasheshe nyingi kiasi cha Yanga sc kukimbilia kushtaki katika mahakama ya usuluhishi wa kesi za michezo duniani(Cas).

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala