Connect with us

Makala

Aucho Nje Wiki Moja

Taarifa kutoka klabu ya Yanga sc zinasema kuwa kiungo Khalid Aucho atakosekana kwa muda wa wiki moja kufuatia kupata majeraha ya mguu baada ya kufanyiwa vipimo kwa kina na kugundulika anahitaji wiki moja ya mapumziko kabla ya kurejea tena uwanjani.

Kwa mujibu vipimo vilivyosimamiwa na Daktari wa klabu ya Young Africans, Moses Atutu ambapo vilionesha kuwa Aucho hajavunjika bali mshipa wa mguu umevimba baada ya mshituko alioupata akiwa mazoezini.

“Mwanzo tulidhani shida ni kubwa kidogo lakini baada ya vipimo tumegundua kuwa hajavunjika bali ni mshipa tu umevimba”Alisema Dk.Moses Atutu.

Awali taarifa zilisema kuwa mchezaji huyo amegoma kurejea uwanjani kwa kuwa anadai baadhi ya fedha zake za usajili lakini taarifa hizo hazikua na uthibitisho wowote mpaka hii muda mfupi ambapo klabu ya Yanga imethibitisha kuumia kwa staa huyo.

Mchezaji huyo ameibuka kuwa tegemeo la kocha Nasredine Nabi eneo la kiungo la Yanga sc tangu asajiliwe misimu miwili iliyopita akitokea nchini Misri ambapo amekua na mchango mkubwa katika ushindi wa klabu yake ya Yanga sc na tayari klabu hiyo imemuongezea mkataba mpya wa miaka miwili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala