Connect with us

Makala

Azam Fc Yaibamiza Prisons Fc

Klabu ya Azam Fc imefanikiwa kuibuka na alama tatu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons uliofanyika katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam baada ya kuifunga timu hiyo 3-0.

Mchezo huo uliokua wa kasi uliwashuhudia Azam Fc wakipata bao la kwanza kupitia kwa mchezaji wa Prisons Fc Yona ambaye alijifunga dakika ya 5 huku Abdul Sopu akifunga dakika ya 48 kwa shuti kali na kumshinda golikipa wa Prisons Fc huku Kipre Jr alifunga bao la tatu dakika ya 70.

Kufuatia ushindi huo Azam Fc sasa imefikisha alama 43 katika michezo ishirini ya ligi kuu ikiwa katika nafasi ya pili ya msimamo huku Yanga sc ikiwa katika nafasi ya kwanza na Simba sc ikiwa katika nafasi ya tatu huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala